Napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha wazazi na walezi wote, pamoja na wanafunzi wetu wapendwa, katika muhula/ mwaka huu mpya wa masomo. Karibuni sana katika shule yenu.
Wazazi na walezi,
Shule ya Msingi Mwanzugi inatambua kuwa malezi ya mtoto ni jukumu la pamoja kati ya mzazi na shule. Mafanikio ya mwanafunzi huanza nyumbani na kuendelezwa shuleni. Tunawaomba muendelee kushirikiana nasi kwa karibu kwa kufuatilia mahudhurio ya watoto wenu, nidhamu, usafi, pamoja na kuwahamasisha kusoma kwa bidii.
Wanafunzi wapendwa,
Nawakaribisha sana katika muhula/ mwaka huu mpya. Nawahimiza mtumie muda wenu vizuri kusoma, kusikiliza walimu wenu, kuheshimu wazazi, walimu na wenzenu. Nidhamu, bidii na utii ni msingi wa mafanikio. Kumbukeni kuwa elimu mnayoipata leo ndiyo itakayowawezesha kuwa raia bora wa kesho.
Walimu wenzangu,
Nawashukuru kwa moyo wa kujituma na uzalendo wenu. Tuendelee kuwalea watoto hawa kwa upendo, haki na nidhamu. Tufundishe kwa moyo, tukumbuke kuwa sisi ni mfano wa kwanza kwa wanafunzi wetu.
Wazazi,
Tunawahakikishia kuwa shule itaendelea kusimamia kikamilifu taaluma, maadili na usalama wa watoto wenu. Pale changamoto zitakapojitokeza, tushirikiane kwa mazungumzo na ushauri ili kuzitatua kwa manufaa ya mtoto.
Kwa pamoja, tushirikiane kuifanya Shule ya Msingi Mwanzugi kuwa kituo bora cha elimu, nidhamu na malezi mema, tukizingatia kauli mbiu yetu: βElimu ni Mwanga.β
Kwa maneno hayo machache, natamka rasmi kuwa Shule ya Msingi Mwanzugi imefunguliwa kwa muhula/ mwaka wa masomo wa 2026.
Posted on January 14, 2026, 10:12 am
Tupo tayari tupeleke shule
Posted on January 12, 2026, 11:24 am
Tunawatakia Heri ya Mwaka Mpya
Posted on December 31, 2025, 11:02 pmHappy birthday Mwalimu Goodluck Mjule
Posted on December 27, 2025, 1:52 pm
Happy birthday Mwalimu Rashid idd msuya
Posted on December 27, 2025, 1:51 pm
Habari Wazazi/Walezi, Shule ya Msingi Mwanzugi inapenda kukutakia kheri ya siku ya krismas wewe na wapendwa wako. Ahsante kwa kuwa pamoja nasi
Posted on December 25, 2025, 9:56 am
18/12/2025
Posted on December 18, 2025, 8:23 am
Shule imefungw Tarehe 05/12/2025 na itafunguliwa Tarehe 13/01/2026,
hivyo kila mzazi/mlezi hakikisha kipindi cha likizo unafanya mambo yafuatayo kwa mwanao
1.Kumuandalia vifaa vyote vya kujifunzia mfano madaftari,sare za shule ,karamu na vinginevyo
2.Kumfuatilia maendeleo yake baada ya kupokea taarifa ya matokeo na maendeleo yake shuleni
3.Kumlinda na kumuhimiza umuhimu wa shule pia kumtahadharisha na mambo mabaya ya kijamii haswa kipindi hiki cha likizo
4.Siku ya kufungua shule afike kwa wakati ili aweze kuendelea na masomo
Hivyo shule ya msingi mwanzugi inawatakia wanafunzi wote likizo njema na heli ya Krismass na Mwaka mpya
KWA MAWASILIANO ZAIDI TUPIGIE KWA NAMBA ZIFUATAZO
1.MWALIMU MKUU 0753576431
2.MWALIMU MKUU MSAIDIZI 0621295401
3.MTAALUMA WA SHULE 0627555552
Posted on December 9, 2025, 7:23 pm
Mwalimu mkuu Saidi Hayawi Leo Tarehe 04/12/2025 ameteua kamati mbalimbali za shule.
Kamati hizo zitaanza kazi mara moja kwa ajili ya mwaka 2026
Posted on December 4, 2025, 3:55 pm
Muandikishe mwanao sasa
Posted on November 29, 2025, 9:14 am