Professional Blog Viewer

Browse blog posts clean and secured.

Total Posts
30
Quick and secure filtering

πŸ”– Latest Blog Posts

Showing 7 to 12 of 30 posts
Page 2 of 5

TANGAZO KWA WAZAZI NA WALEZI

πŸ—“ March 28, 2026 at 7:42 am πŸ–Ό Image
Uongozi wa shule unapenda kuwataarifu wazazi na walezi wote kuwa shule imefungwa rasmi jana tarehe 27/03/2026, na itafunguliwa tena tarehe 08/04/2026 kwa ajili ya kuendelea na masomo ya muhula unaofuata.

Kutokana na mwingiliano wa ratiba ya mitihani ya Darasa la Saba (Pre-Mock na Mock ya Wilaya), tunapenda kuwajulisha kuwa mitihani kwa wanafunzi wa Darasa la Awali hadi Darasa la Sita itafanyika wiki ya pili baada ya kufunguliwa kwa shule.

Aidha, tunapenda kuwajulisha kuwa matokeo ya mtihani wa Mock ya Wilaya kwa Darasa la Saba yatatangazwa hivi punde, na yatapatikana kwenye kipengele cha Mock Wilaya 2026.

Uongozi wa shule unaomba radhi kwa usumbufu wowote ulioweza kujitokeza na tunawashukuru kwa ushirikiano wenu endelevu katika kuboresha elimu ya watoto wetu.

Asanteni kwa ushirikiano
Blog image

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

πŸ—“ March 25, 2026 at 1:01 pm πŸ–Ό Image
Tunapenda kukujulisha kuwa kuanzia leo tarehe 25.3.26 mpaka 26.3.2026 tutakuwa na mitihani ya MOCK WILAYA kwa wanafunzi wa darasa la saba na pindi matokeo yatakapo toka tutawajulisha na yatapatakina kupitia mfumo wetu wa matokeo mwanzugi.com
Muwe na siku njema
Blog image

EID MUBARAK

πŸ—“ March 21, 2026 at 12:19 pm 🎬 Uploaded Video
Salamu kutoka kwa mwalimu Mkuu

MICHEZO YA KIRAFIKI

πŸ—“ March 20, 2026 at 3:38 pm β–Ά YouTube Video
Ifuatayo ni Highlights ya michezo mbalimbali iliyochezwa Tarehe 19/03/2026 kati ya Mwanzugi Pr School na St Joseph Pr School katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwanzugi

MATOKEO YA MECHI YA KIRAFIKI

πŸ—“ March 19, 2026 at 8:19 pm πŸ–Ό Image
Haya ni matokeo ya mechi ya kirafiki kati ya Mwanzugi shule ya Msingi na St.Joseph Primary School
Blog image

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

πŸ—“ March 19, 2026 at 11:49 am πŸ–Ό Image
Uongozi wa Shule ya Msingi Mwanzugi unapenda kuwajulisha wazazi, walezi, wanafunzi pamoja na wadau wote wa elimu kuwa kutakuwa na mechi ya kirafiki ya mpira wa miguu kati ya:

Mwanzugi Primary School πŸ†š St. Joseph

πŸ“… Tarehe: (19.03.2026)
πŸ•’ Muda: (saa 5 asubuhi)
πŸ“ Mahali: (uwanja wa mwanzugi sm)

Lengo la mechi hii ni kukuza vipaji vya wanafunzi, kuimarisha afya, nidhamu pamoja na kujenga urafiki na mshikamano kati ya shule hizi mbili.

Pia kutakuwa na burudani mbalimbali kama riadha nk
Hamasa kubwa kutoka kwa mashabiki, pamoja na fursa ya kuona vipaji chipukizi vikionyesha uwezo wao uwanjani.

Karibuni sana tushuhudie mchezo wa kuvutia, wa ushindani wa kirafiki lakini wenye ubora wa hali ya juu!

β€œMichezo ni afya, umoja na furaha kwa watoto wetu.”
Blog image