Professional Blog Viewer

Browse blog posts clean and secured.

Total Posts
30
Quick and secure filtering

🔖 Latest Blog Posts

Showing 19 to 24 of 30 posts
Page 4 of 5

MAIMUNA JUMA ABDALAH NI MWANAFUNZI WA DARASA LA SABA

🗓 March 16, 2026 at 1:12 am 🎬 Uploaded Video
Akiwashukuru Shirika la UNICEF kwa msaada waliotoa kwa kuwapatia Begi,Daftari,Karamu na vifaa vingine wanafunzi wa Memkwa

MWALIMU DANIEL CHACHA

🗓 March 16, 2026 at 1:05 am ▶ YouTube Video
Mwlimu Daniel Gailigi Chacha akifundisha darasa la kwanza sauti za herufi kutoka shule ya msingi Mwanzugi

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

🗓 March 14, 2026 at 3:10 pm 🖼 Image
Tunapenda kuwataarifu kuwa matokeo ya jaribio la mwezi February kwa wanafunzi yameshatolewa rasmi.
Mzazi au mlezi unaweza kuyapata kwa kuingia kwenye mfumo wa shule kupitia tovuti ya mwanzugi.com.
Njia ya kuangalia matokeo:
1. Fungua Google au Chrome kwenye simu yako.
2. Andika mwanzugi.com kisha bonyeza search.
3. Ingia kwenye mfumo wa shule.
Weka jina la mtumiaji (username) na neno la siri (password).
4. Chagua sehemu ya Test 2 ili kuona matokeo ya mwanafunzi ya mwezi February
Kwa msaada zaidi tafadhali wasiliana nasi.

Mwanzugi Primary School
Elimu bora kwa maendeleo ya mwanafunzi.
Blog image

PONGEZI KWA MWL. MSUYA

🗓 March 14, 2026 at 12:56 pm 🖼 Image
🎉 Taarifa ya Pongezi
Tunatoa pongezi za dhati kwa Mwalimu Bora wa Mwezi Februari kwa kujituma kwake katika kutekeleza majukumu ya kufundisha, kuonyesha nidhamu ya hali ya juu pamoja na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya taaluma shuleni.
Mafanikio haya ni ishara ya bidii, uwajibikaji na moyo wa kujitolea katika kazi ya ualimu. Tunamtakia mafanikio zaidi na tunaamini ataendelea kuwa mfano bora kwa walimu wengine.
Hongera sana! 👏📚
Blog image

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

🗓 March 14, 2026 at 12:45 pm 🖼 Image
📢 JINSI YA KUPAKUA APP YA MWANZUGI
Ili kuendelea kupata huduma zetu kwa urahisi zaidi, fuata hatua zifuatazo kupakua App ya mwanzugi.com:
1️⃣ Fungua Google Chrome au kivinjari chochote kwenye simu yako.
2️⃣ Andika: mwanzugi.com kisha bonyeza search.
3️⃣ Ukishaingia kwenye tovuti, nenda kwenye kipengele cha “Pakua App”.
4️⃣ Moja kwa moja itaonesha notification ya kudownload.
5️⃣ Baada ya kukamilika, App itaonekana kwenye uwanja wa app zote (App Menu) kwenye simu yako.
Pakua sasa na ufurahie huduma kwa haraka, salama na kwa urahisi zaidi.
Blog image

TAARIFA KWA WAZAZI NA WALEZI

🗓 March 14, 2026 at 12:33 pm 🖼 Image
Kwa heshima na taadhima kubwa, Uongozi wa Shule unapenda kuwajulisha kuwa katika kuendeleza uwazi, uwajibikaji na ufuatiliaji wa maendeleo ya kitaaluma ya wanafunzi, matokeo ya Jaribio la Mwezi Februari kwa Darasa la Tatu hadi la Saba yatatolewa muda wowote kuanzia sasa kupitia mfumo wetu rasmi wa mwanzugi.com.
Tafadhali ingieni kwenye akaunti zenu za mfumo huo ili kuyatazama na kufuatilia maendeleo ya mtoto wako. Endapo utapata changamoto yoyote ya kiufundi, usisite kuwasiliana na ofisi ya shule kwa msaada zaidi.
Tunathamini sana ushirikiano wenu endelevu katika kukuza na kuimarisha taaluma ya watoto wetu. Ushirikiano wenu ni msingi imara wa mafanikio yao.
Kwa niaba ya Uongozi wa Shule.
Blog image